TAARIFA
🗓 August 16, 2025 at 8:34 am
TAARIFA
Tarehe 15/08/2025, siku ya Ijumaa, katika Shule ya Msingi mwanzugi kimefanyika kikao cha tathmini ya kazi za kila idara kwa kipindi cha Julai – Agosti 2025.
Kikao hiki kililenga kupitia mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha utendaji katika kipindi kijacho. Viongozi wa idara mbalimbali walitoa taarifa zao na mjadala wa pamoja ulifanyika kwa lengo la kuinua kiwango cha taaluma na maendeleo ya shule kwa ujumla.
Kwa pamoja, kikao kiliwahimiza walimu na wafanyakazi wote kuendelea kushirikiana, kuongeza bidii na kuhakikisha shule inaendelea kuwa mfano bora katika elimu na malezi ya mtoto.
Kikao hichi kiliongozwa na:
MWL MKUU: SAID MUNENE